General News

Dr. Mwigulu directs schools to allow exam access despite fee arrears

Prime Minister Dr. Mwigulu Nchemba has directed educational institutions to stop blocking students from taking exams over unpaid fees, while promising increased government loan support.

Asema Serikali itaendelea kuongeza fedha za mikopo ya elimu ya juu WAZIRI MKUU Dkt.. Mwigulu Nchemba amezitaka taasisi za elimu nchini kutowazuia wanafunzi kufanya mitihani ya masomo yao kwa kushindwa kulipa ada.. Pia, Waziri Mkuu amesema Serikali itaendelea kuongeza fedha za mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu na vyuo vya kati ili wanafunzi wengi zaidi wanufaike na mikopo hiyo.. Mheshimiwa Dkt.. Mwigulu ametoa maelekezo hayo leo (Alhamisi Mei 14, 2026) Bungeni jijini Dodoma katika

kipindi cha Maswali kwa Waziri Mkuu wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Latifa Khamis Juwakali aliyetaka kujua mkakati wa Serikali kiuhusu wanafunzi wanaozuiwa kufanya mitihani kwa kutokulipa ada.. Waziri Mkuu amezihimiza taasisi za elimu kuzingatia utaratibu ambao umekuwa ukitumika wa kutowazuia wanafunzi kufanya mitihani.. “Mitihani ni jambo la maandalizi, mwanafunzi anakuwa ameshajiandaa, yupo tayari kwa mitihani na jambo la ada siyo la kwake, kwahiyo anapata adhabu kutokana na hali halisi ya kimaisha ya

familia yake, hili ni jambo ambalo si jema.. Waziri Mkuu ameongeza kwa kusema “turejee kwenye ule utaratibu ambao mitihani ikifika wanafunzi wafanye mitihani, wapimwe, kwa sababu hawapimwi kwa ada, wanapimwa kwa maandalizi ya mafunzo waliyoyapata na utaratibu ule wa kwamba atakapohitaji cheti chake lazima awe amemaliza mahitaji yote ya kimalipo ambayo alitakiwa kuyafanya.” Pia, Waziri Mkuu amezitaka taasisi hizo kuendelea kuwashirikisha na kuwakumbusha wazazi mara kwa mara kwamba kuna mahitaji ya kifedha ambayo wanafunzi hawajayamalizia

ili walipe bila kuathiri masomo ya wanafunzi.. “Anayelipa ada ni mzazi, siyo mwanafunzi, jukumu la mwanafunzi ni kusoma, pamoja na ukweli kwamba vyuo vinatakiwa kupata fedha ili viweze kujiendesha lakini ufanyike utaratibu mzuri kama ilivyokuwa ikifanyika.” Akizungumzia kuhusu mikopo ya elimu ya juu, Waziri Mkuu amesema Serikali itaendelea kuongeza fedha kwani tangu Serikali ya Awamu ya Sita iingie madarakani fedha zimeongezeka mara mbili kutoka shilingi bilioni 400 hadi shilingi bilioni 900.. Katika hatua nyingine, Waziri

Mkuu Dkt.. Mwigulu Nchemba amewahimiza waliowahi kunufaika na mikopo hiyo kurejesha kwa wakati ili wanafunzi wengi zaidi waweze kunufaika.

Dr. Mwigulu, school fees, education loans, student exams, higher education, Tanzania education policy

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Are you human? Please solve:Captcha