Waziri Kombo Attends SADC Emergency Ministerial Meeting

Tanzania's Foreign Minister Mahmoud Thabit Kombo participated in an emergency SADC ministerial meeting in Nairobi to address regional security threats.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), ameshiriki Mkutano wa Dharura wa Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya Siasa, Ulinzi, na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC-MCO), uliofanyika tarehe 10 Mei, 2026, Jijini Nairobi, Kenya.. Mkutano huo uliolenga kuimarisha misingi ya amani, umeongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe.. Dkt.. George Chaponda, ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa wa Jamhuri ya Malawi.. Katika mazungumzo hayo, Mawaziri wamejadili changamoto mbalimbali za kiusalama zinazoikabili kanda hiyo ikiwemo Vurugu zinazoendelea nchini Afrika Kusini dhidi ya raia wa nchi nyingine za Afrika.. Kwa Upande wake Mwenyekiti Dkt.. Chaponda amewahakikishia wajumbe wa mkutano huo kuwa mapendekezo yote yaliyofikiwa yatafanyiwa kazi kwa haraka na kwa ufanisi.. Hatua hii ni sehemu ya mikakati ya SADC kuhakikisha kuwa Kanda ya Kusini mwa Afrika inasalia kuwa kisiwa cha amani, utulivu, na
ushirikiano wa kiuchumi.
Waziri Kombo, SADC, Nairobi meeting, regional security, Mahmoud Thabit Kombo, Southern Africa, diplomacy