tanzania news

Simanjiro land protection calls by Ole Millya

Deputy Foreign Minister James Ole Millya urges Simanjiro pastoralists to protect their land from illegal brokers as development projects move forward.

Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Simanjiro NAIBU Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, James Ole Millya ameiaka jamii ya kifugaji kulinda na kuitunza ardhi yao na kuepuka uuzaji holela wa ardhi.. Ole Millya ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Simanjiro ameeleza hayo kwenye maadhimisho ya wiki ya wazazi wilaya ya Simanjiro iliyofanyika katika kata ya Ruvu Remit.. Amesema wana Simanjiro wanapaswa kuilinda ardhi yao na kutowaachia madalali wa ardhi ambao huwa

wanajinufaisha kwa kuuza.. Amesema jamii ya wafugaji wanatambua kuwa ardhi yao ndiyo kimbilio lao katika kulisha mifugo hivyo wasicheze nayo zaidi ya kuitunza.. “Katika maisha yangu nitapambania ardhi ya wafugaji wa Simanjiro mniunge mkono na tumuunge mkono Rais Samia Suluhu Hassan kwani anatupenda wafugaji,” amesema Ole Millya.. Amesema kila mara amekuwa akieleza bayana kuwa atasimama kidete katika kupiga vita uuzaji holela wa ardhi ya wafugaji wa Simanjiro.. “Tatizo la kutafsiri mipaka ya ardhi ya Simanjiro

na Kilindi kupitia mikoa ya Manyara na Tanga nimeifikisha kwa Waziri Mkuu Mwigulu Nchemba na ameahidi kutuma timu ya uchunguzi,” amesema Ole Millya.. Amesema walanguzi wa ardhi wanatumia tafsiri ya mipaka isiyo sahihi kuuza ardhini ila timu hiyo ya Waziri Mkuu itafika na kutafsiri mipaka ipasavyo.. Katibu tawala wa wilaya ya Simanjiro, DAS Warda Abeid Maulid amesema jamii ya wafugaji inapaswa kupendana na kuachana na migogoro ya ardhi.. “Nawapa salamu za mkuu wa wilaya yetu

Fakii Lulandana kuwa tujikite kwenye shughuli za maendeleo na siyo kujihusisha na migogoro ya ardhi,” amesema Warda.. Katibu wa jumuiya ya wazazi wa CCM wilaya ya Simanjiro, Mirumbe Sasi amesema katika maadhimisho hayo wamegawa taulo za kike kwa wanafunzi wasichana wa shule ya sekondari Ngage na kupanda miti 50.. Sasi amesema pia kulikuwa na mashindano ya kwaya mbili za Ruvu Remit na Edonyongijape, kufukuza kuku na kuvuta kamba.. Diwani wa kata ya Ruvu Remit Yohana

Maitei (Kadogoo) ameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwani hana miradi kiporo iliyobaki.. Kadogoo amesema miradi yote imekamilika na hivi karibuni Ole Millya aliwapatia Sh2 milioni za ununuzi wa madawati katika shule ya sekondari.. “Tuna changamoto ya daraja la mpaka wa Simanjiro na Same mkoani Manyara, tulitoa kiwanja ili kituo cha afya kijengwe ila ni kimya hadi sasa na bwawa la Relumo la Kapoko limekatika na mafuriko yanaathiri Ruvu,”

amesema.

Simanjiro, Ole Millya, land protection, pastoralists, Tanzania development, Ruvu Remit

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Are you human? Please solve:Captcha


Secret Link