tanzania news

ACT Wazalendo yaitaka Serikali kupunguza tozo za mafuta

Chama cha ACT Wazalendo kimeiomba Serikali kuondoa Sh. 500 kwa kila lita ya mafuta ili kupunguza gharama za maisha zinazowakabili wananchi wa kipato cha chini.

Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar es Salaam WAKATI wananchi wakilalamikia kupanda kwa gharama za maisha nchini, Chama cha ACT Wazalendo kimeitaka Serikali kuondoa angalau Sh.. 500 katika kodi na tozo za mafuta kwa kila lita ili kupunguza mzigo unaoendelea kuwaathiri wananchi wa kipato cha chini.. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mai 8,2026 Mwenyekiti wa ngome ya vijana ya ACT Wazalendo, Abdul Nondo amesema ongezeko la bei ya mafuta limeendelea kuchochea kupanda

kwa nauli za usafiri, bei za vyakula na huduma nyingine muhimu huku wananchi wengi wakishindwa kuhimili hali hiyo.. Amesema kwa sasa jumla ya kodi na tozo katika lita moja ya petroli na dizeli zimefikia zaidi ya Sh.. 1,100, hali ambayo imechangia bei ya mafuta kuendelea kuwa juu katika soko la ndani licha ya malalamiko ya wananchi kuongezeka.. “Tunaiomba Serikali iondoe angalau sh.. 500 katika kodi na tozo za mafuta kwa kila lita ili kupunguza ukali

wa maisha kwa wananchi na kushusha gharama za bidhaa muhimu,” amesema Nondo.. Mbali na kupunguza tozo, amesema chama hicho pia kinashauri serikali kutoa ruzuku ya mafuta ya angalau Sh.. 400 kwa kila lita ili kusaidia kupunguza athari za mfumuko wa bei unaoendelea kujitokeza katika sekta mbalimbali za uchumi.. Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2015 (The Petroleum Act, 2015), Kifungu cha 166 kinaeleza kuwa bei za mafuta zitasimamiwa kwa mfumo wa soko lakini

chini ya usimamizi wa mamlaka husika.. Aidha, Kifungu cha 167 cha sheria hiyo kinna eleza kuwa serikali kupitia waziri mwenye dhamana ya mafuta kwa kushirikiana na waziri wa fedha wana mamlaka ya kuweka au kurekebisha tozo za mafuta nchini .. Wachambuzi wa uchumi wanaeleza kuwa kifungu hicho kinaipa serikali nafasi ya kupunguza baadhi ya tozo pale hali ya uchumi inapokuwa ngumu kwa wananchi.. Baadhi ya wananchi waliozungumza na TimesMajira wamesema kupanda kwa bei ya mafuta

kumeongeza kwa kasi gharama za usafiri na bidhaa za vyakula, huku wafanyabiashara wadogo wakieleza kuwa hali hiyo imepunguza uwezo wa wananchi kununua bidhaa sokoni.. Kwa mujibu wa taarifa za Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji (EWURA), mabadiliko ya bei za mafuta nchini hutokana na bei ya mafuta katika soko la dunia, gharama za usafirishaji, thamani ya dola ya Marekani pamoja na kodi na tozo za ndani zinazotozwa katika kila lita ya mafuta..

Wakati huo huo, ACT Wazalendo kimepongeza viongozi na wanachama wake kwa maadhimisho ya miaka 12 ya chama hicho yaliyofanyika kitaifa katika Jimbo la Kilwa Kusini Mei 5, 2026, huku kikisema kitaendelea kuisimamia serikali katika masuala ya uchumi na ustawi wa wananchi.

ACT Wazalendo, bei ya mafuta, tozo za mafuta, gharama za maisha, Serikali ya Tanzania

Secret Link